TIMU YA TAIFA YA KOMORO YAPANDA VIWANGO VYA FIFA
Timu ya Taifa ya soka ya Komoro, imeruka nafasi 9 hadi nambari 119, katika orodha ya viwango bora vya FIFA.
Hii ni baada ya kuwa na mwezi bora zaidi wa kujipa ushindi dhidi ya Ghana na Jamhuri ya Afrika ya kati CAR.
Komoro imeingia nafasi ya 119, ambayo ni nafasi yao ya juu kabisa kwenye orodha ya timu za taifa za FIFA.
Kulingana na orodha, Komoro ni bora kuliko Tanzania, Ethiopia, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, na Niger.
Ushindi huo dhidi ya Ghana na Jamhuri ya Afrika ya kati CAR, umeipa pointi 6 na kuwa kileleni Kundi I.
Kwa kweli, mwezi huu wa Novemba ni mwezi wenye furaha zaidi kwa Komoro, na macho yote sasa yako kwenye timu hiyo kuona ikifanya vizuri zaidi siku za hivi karibuni.
Timu ya taifa ya soka ya Komoro, maarufu ‘Coelacanthes’ imepewa jina hilo baada ya aina ya samaki, ‘Coelacanthes’.
Kuna aina mbili tu za samaki za ‘coelacanths’ zinazojulikana: na moja inapatikana Visiwa vya Comoros, pwani ya mashariki ya Afrika.