Michuano ya kombe la Mataifa ya Amerika ya Kusini, Copa America 2024 imeendelea usiku wa kuamkia leo Juni 25, 2024 ambapo katika mchezo uliomalizika alfajiri hii, timu ya Taifa ya Brazil imelazimishwa sare tasa dhidi ya Costa Rica katika mchezo wa raundi ya kwanza wa Kundi D uliopigwa katika dimba la SoFi Stadium (Inglewood, CA).

Sare hiyo inaifanya Costa Rica kuweka rekodi ya kuepuka kipigo dhidi ya Brazil kwa mara ya kwanza tangu 1959 kufuatia vipigo 10 mfululizo.

Katika mchezo wa mapema wa Kundi D, kiungo wa zamani wa Real Madrid, James Rodriguez ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mechi akitoa asisti mbili katika ushindi wa 2-1 wa Colombia dhidi ya Paraguay.

Mabao ya Colombia yametiwa kimiani na nyota wa Crystal Palace, beki Daniel Munoz na kiungo Jefferson Lerma huku bao la kufutia machozi la Paraguay likifungwa na winga wa Brighton, Julio Enciso.

FT: Colombia 2-1 Paraguay

⚽ Munoz 32'

⚽ Lerma 42'

⚽ Enciso 69'


FT: Brazil  0-0  Costa Rica

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement