Michuano ya Copa America 2024 imeendelea tena alfajiri ya leo Juni 26, 2024 kwa mechi mbili ambapo bingwa mtetezi, Argentina ameibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Chile katika dimba la MetLife, New Jersey na kutinga hatua ya robo fainali.


Bao la pekee la Argentina limetiwa kimiani na mshambuliaji wa Inter Milan, Lautaro Martinez jioni kabisa dakika ya 88 ya mchezo.

Katika mchezo mwingine wa kundi A, Canada imeweka matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Peru huko Kansas City huku bao pekee likifungwa na mshambuliaji wa Lille, Jonathan David mnamo dakika ya 74.


FT: Chile 0-1 Argentina

⚽ Martinez 88’

FT: Peru 0-1 Canada

⚽ David 74’


MSIMAMO KUNDI A baada ya mechi mbili 

Argentina — 6

Canada — 3

Chile — 1

Peru — 1

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement