Juventus na Bernardo Silva

Klabu ya Juventus imeweka wazi dhamira ya kumnyakua kiungo wa kati wa Ureno, Bernardo Silva (31), mara tu mkataba wake na Manchester City utakapoisha msimu ujao wa joto. Endapo dili hilo litafanikiwa, nyota huyo ataondoka Etihad bila ada ya uhamisho.


 Man City na Kobbie Mainoo


Kwa upande mwingine, Manchester City wanaripotiwa kumvizia kiungo chipukizi wa Manchester United, Kobbie Mainoo (20). Hata hivyo, City huenda wakakabiliwa na ushindani mkali kutoka Chelsea na Newcastle ambao pia wanamtamani kiungo huyo wa timu ya taifa ya England.


 Chelsea na Rogers


Chelsea hawajakata tamaa kwa mshambuliaji wa Aston Villa, Morgan Rogers (23). Ingawa ada ya uhamisho inayokisiwa kufikia paundi milioni 80 imewaudhi viongozi wa Stamford Bridge, klabu hiyo bado inavutiwa na mchezaji huyo.


 Ruben Amorim na Manchester United


Imefichuka kuwa kocha Ruben Amorim atapokea fidia ya takribani paundi milioni 12 endapo Manchester United watamfukuza kabla ya kutimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe rasmi, tarehe 1 Novemba. Wakati huohuo, ripoti za kifedha zilizotolewa karibuni zimeongeza matumaini ya United kumnasa kiungo wa Brighton na Cameroon, Carlos Baleba (21).


 Crystal Palace na Christantus Uche


Mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa Nigeria, Christantus Uche (22), kutoka Getafe kwenda Crystal Palace una kipengele cha kuwa wa kudumu ikiwa ataanza michezo 10 msimu huu.


 Liverpool na Ronald Araujo


Liverpool wanadaiwa kuandaa dau la euro milioni 50 (sawa na paundi milioni 43.35) kwa ajili ya beki wa Barcelona, Ronald Araujo (26). Tottenham nao wameonyesha nia ya kumuwania mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay.


 Birmingham na Alfie Smith


Klabu ya Birmingham inataka kumfunga mkataba mpya kipa kinda wa Uingereza chini ya miaka 15, Alfie Smith (14), ili kuzima nia ya vilabu vikubwa kama Chelsea, Arsenal, Liverpool, Manchester United na Manchester City.


 Chelsea na Marc Guehi


Chelsea imeingia rasmi katika kinyang’anyiro cha kumsajili beki wa kati wa England, Marc Guehi (25), mara tu mkataba wake na Crystal Palace utakapokoma msimu ujao

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement