TENIS : MMAREKANI AMTWANGA SABALENKA NA KUTINGA FAINALI
Amanda Anisimova amemshushia kichapo na kumwondoa mcheza tenis namba moja kwa ubora Duniania, Aryna Sabalenka, na kufanikiwa kufika fainali ya muchuano ya Wimbledon kwa upande wa wanawake.
Ilikuwa siku bora zaidi kwa Anisimova, anayeshikiria nafasi ya 13 kwenye viwango vya ubora duniani, kwa upande wa wanawake, akishinda seti 6-4 4-6 6-4, mbele ya Sabalenka katika mtanange uliochukua masaa mawili na dakika 35.
Hata hivyo baada ya mchezo alieleza furaha yake juu ya ushindi huo huku akimwaga sifa kwa Sabalenka"Haikuwa rahisi. Kama siamini hivi, ni kama nilikuwa nakufa uwanjani leo.”
Fainali ya wanawake itakuwa Anisimova dhidi ya Świątek, na itachezwa Jumamosi, 12 Julai 2025, kwenye uwanja wa Centre Court .