Sergio Busquets Ajiunga na Lionel Messi katika klabu ya Inter Miami
Sergio Busquets amejiunga na Inter Miami kama mchezaji huru, klabu hiyo ilitangaza Ijumaa hii. Kiungo huyo wa kati wa zamani wa Barcelona na Uhispania, 34, ataungana tena na rafiki yake na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barca Lionel Messi baada ya kutoongeza mkataba wake Camp Nou baada ya kukaa kwa miaka 18.