Rais wa Yanga, Said Hersi amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Vilabu Afrika (Africa Clubs Association-ACA) katika uchaguzi uliofanyika Cairo nchini Misri.

Hersi ameweka rekodi ya kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa asasi hiyo ambayo imezinduliwa leo na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe.

ACA ina lengo la kuunganisha wadau kutoka kote katika tasnia ya soka Afrika, kukuza ushirikiano, ubunifu, na ufanisi ndani ya eneo la vilabu vya soka barani Afrika.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement