Rais wa baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati "CECAFA" Wallace Karia ameziomba nchi wanachama wa ukanda huo kupangilia ratiba zao ili kuendana na mashindano ya CECAFA Kagame Cup ambayo yatakuwa na Muendelezo Kila mwaka.

Rais Karia ameweka wazi kuwa lengo ni kuhakikisha wanakuwa na kuendelezo mzuri zaidi kunako Michuano hiyo sambamba na kutoka pongezi kwa Rais wa Rwanda na mdhamini Mkuu wa mashindano hayo Paul Kagame kwa kuchaguliwa kuendelea kuongoza Taifa hilo.

Rais Karia amezungumzia pia mechi za Nusu Fainali Michuano ya CECAFA Dar Port Kagame Cup 2024 zitakazopigwa Leo ikiwakutanisha APR ya Rwanda dhidi ya Al Hilal huku Hay Al Wadi Fc wakivaana na Red Arrows huku akitoa pongezi na shukrani kwa wamiliki wa Uwanja wa KMC.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement