Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewataka wachezaji wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifs Stars” kutuma ujumbe Duniani kwa kuhakikisha wanalipambania Taifa katika mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Zambia wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia kwa nchi za Afrika utakaopigwa hii leo dimba la Levy Mwanawasa nchini humo.

Waziri Ndumbaro amezungumza na wachezaji hao ikiwa ni sehemu ya kuwasilisha Ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye ameahidi kuwazawadia shilingi milioni 100 iwapo watapata ushindi katika mchezo huo huku akiweka Shilingi Milioni 10 kwa kila Goli ikiwa ni sehemu ya Goli la Mama.

“Ni mechi muhimu sana kwetu, mechi ambayo tutakwenda kutuma ujumbe Duniani, na yoyote atakayepangwa na Kocha kuanza ajue anawakilisha Watanzania Milioni 62, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuanzia Dakika ya kwanza mpaka ya tisini atakaa kwenye Telivishion kuangalia watoto wake, ameweka Goli la Shilingi Milioni 10 kwa kila goli lakini ameniagiza tena endapo tutashinda mechi hii anaweka mezani Shilingi Milioni 100, huo ni upendo wa Mheshimiwa Rais wa nyinyi watoto wake, wajukuu zake, ” Amesema, Waziri wa Michezo Dkt: Damas Ndumbaro.

Waziri Ndumbaro ameongeza kwa kuwataka wachezaji kujituma zaidi kuhakikisha Tanzania inazidi kujitangaza kimataifa kupitia michezo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement