Timu ya PETRO DE LUANDA ya Angola imechukua taji lake la kwanza la ligi kubwa ya kikapu barani Africa baada ya kiufunga AL AHLY LY ya libya kwa points 107-94 siku ya jumamosi na kuingia katika rekodi ya kua bingwa baada ya kuzishinda klabu kubwa kama Zamaleki,Al ahly Cairo na Us monastir ya Tunisia.

Mashindano haya ya BAL yaani basketball Africa League yalianzishwa mwaka 2019 na mpaka sasa kila mwaka umetoa bingwa mpya hakuna ambae amefanikiwa kuchukua kombe hili mara 2 bali wamekua wakigawana kuchukua taji hili. 

Mashindano haya ya BAL yametawaliwa Zaidi na TIMU kutoka ukanda wa kaskazini wakiwa wamechukua mara nyingi zaidi kuliko ukanda mwingine wowote ule barani Africa, na timu hizo ni kama Al ahly Cairo,Zamarek Cairo na Us monastir ya Tunisia ambazo zote niza kaskazin mwa Africa. 

Lakini pia michuano hii tumeshuhudia klabu ya Rivers Hoopers kutokea Nigeria waliweza kushika nafasi ya 3 baada ya kuifunga timu ya Cape Town tigers ya pale South Africa kwa points 80-57. 

Hata hivyo kumekua na mjadala kwanini tumekua hatupati timu kutoka Africa mashariki kuweza kua bingwa shida ni nini wakati ukienda pale Rwanda timu kama REG,APR,PATRIOTS,UGB, KIGALI TITANS Nk, zina uwezo mkubwa sana lakini uwekezaji mkubwa sanaa maana ligi yao imeanza mwaka 1977 lakin pia mataifa jirani kama Burundi,Kenya,Uganda, DRC na Sudan hazifanikiwi kwenye michuano hii ya BAL. 

PETRO DE LUANDA imefanya mapinduzi makubwa chini ya kocha Sergio Valdeolmillos kutoka Spain amekua bora kwenye mbinu na sistimu yake jinsi ya kuzuia na kushambulia amekua bora sanaa na malengo yao ni kuhakikisha wanatawala ligi hii ya BAL kumbuka timu hii Petro de LUANDA imeanzishwa mwaka 14 January 1980.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement