Nyota wa Yanga, Pacome Peodoh Zouzoua amejumuishwa kwenye kikosi cha awali cha wachezaji 53 wa Ivory Coast "The Elephant' kitakachoingia kambini kuipambania bendera ya nchi hiyo kwenye michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza Januari 13 hadi Februari 11, 2024.

Katika kikosi kilichosheheni mastaa wanaocheza katika Ligi mbalimbali za Ulaya, Asia na Afrika, Pacome ndiye mchezaji pekee ambaye anatoka kwenye Ligi ya Tanzania Tangu ajiunge na Yanga, Pacome amefunga mabao manne kwenye Ligi Kuu Bara na matatu kwenye michezo minne ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kushika nafasi ya pili katilka orodha ya ufungaji bora akishindana na Sankara Karamoko wa ASEC Memosas anayeongoza akiwa na manne.

Mastaa wengine walioitwa kwenye kikosi hicho ni Seko Fofana wa Al Nassr, Wilfred Zaha wa Galatasaray, Hamed Traore wa Bournemouth, Sebastian Haller wa Borussia Dortmund, Amnad Diallo wa Manchester United, Idrisa Doumbia wa Al Ahly, na Antony Urbain wa ASEC Memosas.

Ivory Coast ipo kundi A kwenye michuano hiyo ikiwa na Nigeria, Equatorial Guinea na Guinea Bissau.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement