"Makipa wakubwa waliowahi kuhudumu katika klabu ya Manchester United kama Schmeichel na De Gea hawakuanza vizuri sana".

"Kwa Andre Onana ni vizuri kujua historia kidogo. Anajua kama sisi tunafahamu kuwa atafanya vizuri zaidi."

Msururu wa makosa yameangaziwa katika mwanzo mgumu wa United kwenye kampeni - ya hivi punde zaidi katika ushindi dhidi ya Brentford wiki mbili zilizopita wakati mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon aliposhindwa kushuka chini haraka na kuzuia bao la Mathias Jensen kipindi cha kwanza.

"Ten Hag anakubali kuwa uwezo wa golikipa wake Andre Onana haijakuwa nzuri vya kutosha lakini kuna uhakika kwamba mchezaji huyo ataendelea kuimarika".

"Kila mchezaji anayekuja kwenye Ligi kuu ya England anahitaji muda wa kuendana na mazingira".

"Nina uhakika Andre Onana atafanya vizuri na nina hakika tutakuwa na furaha nyingi pamoja naye."

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement