Kocha wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspur ya nchini England, Nuno Espirito Santo. Amefutwa kazi na klabu ya Al Ittihad inayoshiriki Ligi kuu ya Saudi Arabia, kufuatia mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha.

Santo, aliiongoza Al Ittihad kutwaa taji la Ligi msimu uliopita, lakini kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Al Quwa ya Iraqi katika michuano ya klabu Bingwa barani Asia siku ya Jumanne, kimewafanya viongozi wa klabu hiyo kuchukua hatua ya kumpiga kalamu. Na sasa nafasi ya ukocha Mkuu katika kikosi hicho, itakaimiwa na aliyekuwa kocha msaidizi, Hassan Khalifa wakati timu hiyo ikiendelea kumtafuta mbadala wa kudumu.

Ikumbukwe, pamoja na kufanya usajili wa wachezaji nyota kama Karim Benzema kutoka Real Madrid na Ng'olo Kante, baada ya michezo 12 Al Ittihad wanashika nafasi ya sita katika msimamo wa Saudi Pro League. Wakiwa na alama 11 pungufu ya Al Hilal wanaoongoza!

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement