MWAMUZI KUTOKEA TAIFA LA PERU AONYESHA UBAGUZI KWENYE MCHEZO WA COPA AMERICA
Mwamuzi wa kati(Refaree) kutokea taifa la Peru bwana mdogo Kevin Ortega Pimentel miaka 32 ambae alianza kuchezesha ligi kuu ya Peru(Peruvian Primera Division) mwaka 2015 lakini kukabidhiwa badge ya fifa mwaka 2019 ameweza kuzua TAHARUKI kubwa ya ishara ya kibaguzi kwenye Mchezo wa group C mzunguko wa 3 wakutamatisha kundi.
SASA katika kundi hilo C mchezo uliofanyika leo alfajiri kati ya USA na Uruguay ambapo tumeshuhudia Uruguay ameshinda goli 1 nakufanya Uruguay akishinda michezo yote 3 kwenye kundi lake na kufikisha alama 9 na kwenda Robo fainali lakini pia kuweka REKODI mpya tangu mwaka 1916 Uruguay kushinda michezo yote kwenye kundi
Bwana mdogo Kevin Ortega Pimentel alimbagua mchezaji wa USA mr Christian Pulisic ambae alienda kumpa Mkono refa huyo kwa bahati mbaya refa huyo akagoma kabisa kutoa Mkono kitu ambacho kimeonesha ubaguzi tena kwa refa ambae alipaswa kutoa mkono kwa ishara ya uungwana lakini bwana mdogo Kevin Ortega Pimentel amegoma kabisa
Sababu ambayo inatajwa ni kwamba wakati Uruguay wanapata bao captain wa USA Mr Christian Pulisic alitoa neno ambalo si zuri akisema 'Haya nenda kashangilie hilo goli na Uruguay' huenda kauli hii ilimkela refa huyu na kuliweka kiporo ndio maana alimnyima Mkono.
Pia refa huyo Kevin Ortega Pimentel amepitia matukio mbali mbali kama vile mechi ya Universitario De Deportes vs Cienciano alishindwa kutafsiri vyema penati lakini 2022 mechi ya Copa Libertadores mechi kati ya Boca Juniors vs Club Always Ready pia alitereza kwenye kuamua tena kwa mara nyingine lakini pia tuhuma nyingne refa huyo Kevin Ortega Pimentel aliwahi kutwa na jezi ya Boca Juniors na askari police kwenye kibanda chake