MVUTANO kati ya Wizara ya Michezo na Shirikisho la soka la Cameroon umeleta mgawanyiko kwa wapenda soka wa nchi hiyo wakijiuliza hatma ya soka lao katika siku zijazo.

Wakati Waziri wa Michezo akimtangaza, Mbelgiji Marc Brys kama Kocha wa timu ya Taifa ya Cameroon wiki moja iliyopita, Rais wa F├ęcafoot alimetangaza kumteua ifikapo Jumanne Aprili 9 Meneja mwingine wa kiufundi wa timu ya Taifa. 

Baadhi ya raia wanapongeza hatua hiyo ya Waziri wa Michezo ya kufanya uteuzi wakidai kuwakilisha Mamlaka Serikali huku wengine wakisema kuwa anatumia nguvu aliyonayo kufanya maamuzi kitu ambacho kinaweza kuleta athari kubwa kwa Cameroon.

Wafanyakazi walioteuliwa na Waziri wa Michezo wanapaswa kuapishwa kufikia Jumanne, siku hiyo hiyo ambayo Samuel Eto'o atakapofanya uteuzi wake.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement