Lionel Messi, alfajiri ya leo ameweka rekodi mpya Katika historia ya soka na mashindano makubwa ya copa america mara baada ya kukanyaga nyasi za Mercedes Benz stadium basi Messi amekua mchezaji wa kwanza kushiriki michuano hii mara nyingi Zaidi ikiwa ni mara 7 na michezo 35 

Rekodi hiyo ilianza mwaka 2007 wakati ilikua ndo mara yake ya kwanza kucheza mashindano ya copa america na sasa imepita miaka 17 na Lionel Messi bado ANAZIDI kuweka REKODI ambazo zitaishi milele na kukumbukwa zaidi

KATIKA Mchezo huo wa ufunguzi kati ya Argentina na Canada ulio tazamwa na watu wengi kweli kweli TAIFA la Argentina imeshinda mabao 2 kwa sifuri mabao ya Alvarez na Martinez imetosha Argentina kuanza kwa KISHINDO 

Michuano hii ya mwaka 2024 ni ya 48 tangu yalivyo anza mwaka 1916 imepita miaka 108 na Argentina ndie BINGWA mtetezi je atafanikiwa kubeba msimu na kua TAIFA lenye mafanikio makubwa Sanaa kwenye kombe hili la Copa America kuweza kufikisha mara 16

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement