MCHEZAJI WA ZAMANI WA ARSENAL THIERRY HENRY ATAJWA KUWA MRIDHI WA KOCHA WA TIMU YA TAIFA WALES
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Ufaransa Thierry Henry ni miongoni mwa majina yanayotajwa kuchukua nafasi ya Rob Page kama meneja wa Wales.
Henry, ambaye amewahi kuinoa Monaco na Montreal Impact, anasimamia kikosi cha Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 na anajiandaa kuiongoza timu ya Olimpiki ya nchi yake kwenye Michezo huko Paris mwezi ujao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 46 ana uhusiano na Wales, akiwa amesomea beji zake za ukocha katika shirikisho la Soka la Wales (FAW).
FAW ilimtimua Page Ijumaa iliyopita baada ya kuhudumu kwa miaka mitatu na nusu kufuatia Wales kushindwa kufuzu kwa Euro 2024.
Baraza linaloongoza linapanga kuchukua muda wake kumteua mrithi.
Baadhi ya mabosi wa FAW wana nia ya kuajiri majina makubwa, kama walivyofanya walipomteua nahodha wa zamani wa Wales na Manchester United Ryan Giggs mnamo 2018.
Henry angekuwa uteuzi wa hadhi ya juu zaidi, ikizingatiwa kuwa yeye ni mmoja wa wachezaji bora wa kizazi chake na bado anajulikana kama mchambuzi wa televisheni na pia kocha wa Ufaransa wa Under-21