Mbunge wa Ghana amemuomba radhi mwanasoka wa Uingereza  Harry Maguire kwa kumfananisha na makamu wa rais wa nchi hiyo akiwataja kuwa ni wachezaji duni.

Mbunge huyo mwaka jana alimkosoa Makamu wa Rais Mahamudu Bawumia kwa utendaji duni wa kiuchumi wa Ghana, na kumfananisha na kile alichosema ni uchezaji mbaya wa Maguire kama mchezaji wa kufunga mabao yake mwenyewe.

Lakini siku ya Jumanne, mbunge huyo Isaac Adongo alisema beki huyo wa Manchester United tangu wakati huo amegeuza maisha yake.

“Bwana Spika, sasa naomba msamaha kwa Harry Maguire.Leo, Harry Maguire amepiga kona na yeye ni mwanasoka wa mabadiliko,” alisema bungeni wakati wa mjadala wa bajeti.

Alikosoa utendakazi wa Bw Bawumia kama makamu wa rais na mkuu wa Timu ya Usimamizi wa Uchumi ya Ghana, ambayo alisema imeingiza nchi kwenye madeni zaidi na kuhatarisha utendaji wake wa kiuchumi.

[Harry Maguire] sasa ni mchezaji muhimu wa Manchester lakini kuhusu Maguire wetu [Bw Bawumia] sasa anazurura katika IMF akiwa na kikombe mkononi,” alisema.

Ghana kwa sasa inapitia mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi kuwahi kutokea katika kizazi.

Mwaka jana, mfumuko wa bei ulifikia rekodi ya juu ya 54% - na bado unaendelea kwa zaidi ya 35%.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement