Kuelekea katika mashindano ya Olimpiki 2024 Paris, mazoezi ya mwisho kwaajili ya Sherehe za ufunguzi za Mashindano hayo zimeendelea Mto Seine.

Wajumbe 205 wataandamana kwenye zaidi ya boti 80 kwenye Seine huku ikitajwa kuwa Sherehe itaendeshwa polepole kutoka mashariki hadi magharibi, daraja hadi daraja, ikiruka kilomita sita (maili 3.7) kutoka Pont d'Austerlitz hadi Pont d'IĆ©na.

Mwezi Mei, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitoa tahadhari juu ya tukio hilo la wazi ambalo halijawahi kushuhudiwa, ambalo linatarajiwa kuleta viongozi Takribani 100 kutoka Mataifa tofauti Duniani huku ikielezwa kuwa tukio hilo linaweza kuhamishiwa kwenye sherehe ya kawaida zaidi ya ufunguzi katika Stade de France.

Licha ya wasiwasi wa kiusalama Mkurugenzi Mtendaji wa Sherehe Thierry Reboul alithibitisha kuwa mamlaka bado inajiandaa kwa tukio hilo la kipekee la wazi na kwamba hakuna sherehe mbadala zinazoandaliwa katika hatua hii.

"Kama unavyoona hapa, kuna Seine na kuna boti kwa hiyo inaonekana kama Plan A. Hakika ndiyo tunaifanyia kazi na tunaifanyia mazoezi, kama unavyoona leo.", Reboul alisema.

Tangu mashambulizi ya kigaidi ya mwaka 2015, hali ya usalama inatekelezwa mara kwa mara wakati wa matukio makubwa.

Sherehe inapofanyika kwenye Seine, madaraja kadhaa yatafungwa hatua kwa hatua kwa trafiki ambapo Kutakuwa na mazoezi ya mwisho kabla ya sherehe ya ufunguzi wa Julai 26.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement