MATAIFA YALICHUKUA IDADI KUBWA YA MEDALI ZA DHAHABU OLIMPIKI 2024 PARIS
Baada ya kupitia kwa kipindi kirefu, nchi za Marekani na China zimefungana kwenye medali za dhahabu hadi asubuhi ya leo kila moja ikiwa nazo 21.
Huku nchi ya tatu ambazo ni Ufaransa ikiwa imefungana pia na Australia ambayo ipo nafasi ya nne kila moja ikiwa na medali 13 za dhahabu.
Kufungana huko kumetokea pia kwenye nchi ya tisa na kumi, Uholanzi wakiwa wanashika nafasi ya tisa imefunga na Ujerumani kila moja ikiwa na medali saba za dhahabu, lakini pia nchi hizo zimefungana kwenye medali ya shaba ambapo kila moja imeshatwaa tatu hadi sasa.
Kuanzia nafasi ya 13, nchi nne zimefungana kwenye medali za dhahabu ambazo ni New Zealand, Hungary, Romania na Ireland kwa kila moja imetwaa medali tatu za dhahabu.
Nchi za Afrika ambazo hadi sasa zimechukua medali za dhahabu kwenye mashindano haya ni Afrika Kusini ambayo inashika nafasi ya 29 ikiwa nayo moja, lakini jumla ikiwa imekusanya medali nne.
Kenya ambayo inashika nafasi ya 31 ikiwa na medali moja ya dhahabu lakini jumla imekusanya tatu, Algeria inashika nafasi ya 37 ikiwa na medali moja ya dhahabu ikiwa ndiyo pekee imeitwaa hadi sasa sawa na Uganda inayoshika nafasi ya 37 pia.
Nchi nyingine zenye medali kutoka Afrika ni Ethiopia ambayo imekusanya jumla ya medali mbili zikiwa zote ni za shaba, Tunisia ina moja, Cape Verde moja na Misri moja.