MABONDIA WA UFC WA TIMBA IKULU YA TRUMP
Rais wa Marekani, Donald Trump, amefunguka kuhusu mpango wake wa kuusogeza ‘White House’ mchezo wa Sanaa ya Mapigano Mchanganyiko (UFC), akiwa amedhamiria kufanya hivyo mwakani (2026) katika sherehe za Miaka 250 ya Uhuru wa Marekani.
Trump alishawahi kuonekana katika mapambano kadhaa ya UFC miaka ya hivi karibuni na kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki alioungana nao, huku mabondia wa mchezo huo pia walimpongeza kwa wingi kufuatia ushindi wake kwenye kinyang’anyiro cha Urais.



