Maafisa hao ni Adolphe Kalisa, al maarufu Camarade, ambaye amekuwa katibu mkuu wa shirikisho tangu 2023, na Eric Tuyisenge, ambaye alikuwa msimamizi wa vifaa vya timu ya taifa ya kandanda, Amavubi.

RIB inasema katika uchunguzi wa pamoja na polisi wa kitaifa, waliwafungulia mashtaka maafisa hao wawili kwa makosa ya ubadhirifu, ufisadi na utumiaji wa hati ghushi.

Kalisa na Tuyisenge hawajatoa kauli yoyote hadharani kuhusiana na uhalifu huu unaodaiwa.

Idara ya Upelelezi wa Jinai inasema kuwa faili ya Adolphe Kalisa tayari imewasilishwa kwa upande wa mashtaka ili iweze kufikishwa mahakamani.

Washukiwa hao wawili kwa sasa wanazuiliwa katika kizuizi cha katika vituo vya polisi vya Remera na Kicukiro mjini Kigali.

Makosa kamili wanayoshitakiwa bado hayajawekwa wazi. Hata hivyo, habari zinaendelea kusambaa kwenye vyombo vya habari vya Rwanda kuhusu ubadhirifu wa bajeti ya timu ya taifa ilipokuwa ikishiriki mechi za kimataifa.

Shirikisho la soka la Rwanda ni moja ya taasisi ambazo mara nyingi hupitia mabadiliko ya mara kwa mara katika uongozi.

Mara nyingi kumekuwa na malalamiko kuwa usimamizi wa fedha katika shirika hili sio wazi.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement