Golikipa Lev Yashin alikua na mapenzi makubwa na mchezo wa soka licha ya kupitia changamoto ya kutokubalia zaidi lakini uwezo na jitihada binafsi zimemtambulisha katika uso wa Dunia. 

Alishindwa kuwa golikipa wa mchezo wa mpira wa miguu 1950 na akaenda kujiungana na mchezo wa Hockey. 

Akiwa golikipa kwenye mchezo huo wa Hockey alifanikiwa kunyaua taji la Soviet Cup mwaka 1953. 

Lev Yashin alikua na matarajio makubwa sana na mchezo wa Soka hiyo aliamua kuacha mchezo wa Hockey na kurudi tena kwenye mchezo wa mpira wa miguu. 

Akiwa golikipa wa mpira wa miguu mwaka 1963 Lev Yashin akafanikiwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa Dunia "Ballon D"or 

Mpaka sasa Lev Yashin yupo kwenye historia ya kuwa golikipa pekee aliyewahi kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa Dunia "Ballon D'Or".

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement