Mchezaji LeBron James na timu yake ya Los Angeles Lakers hawafikirii kuwa mchezaji huyo anapata faulo za kutosha kwenye mechi zao kama ambavyo anastahili. Siku moja baada ya mechi ya Miami Heat James na kocha mkuu Darvin Ham walipeleka malalamiko kuhusu staa huyo kuchezewa faulo nyingi kwenye mechi ya Jumatatu ambayo Lakers walipoteza kwa pointi 108-107 dhidi ya Miami Heat.

Lakers waliwasilisha malalamiko rasmi kwenye ofisi ya ligi ya NBA. Kulingana na ripoti hiyo, Lakers walitaja "faulo nyingi ambazo hazikufanyiwa kazi na marefa" zikilenga faulo ambazo amechezewa James. Lakers walipeleka klipu nyingi za mchezo huo kuonyesha wanachopinga ni faulo za wazi dhidi ya James ambazo hazikuitwa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement