Kuelekea katika Michuano ya EURO 2024, Kocha wa Timu ya Taifa ya England Gareth Southgate amesema muda wa mwisho wa kukamilisha kikosi chake kwa ajili ya michuno hiyo.

Uingereza itacheza na Iceland uwanjani Wembley siku ya Ijumaa katika mechi ya mwisho ya kirafiki kabla ya mchuano huo, baada ya hapo Southgate atathibitisha kundi la wachezaji 26 atakalopeleka Ujerumani.

Akizungumzia uteuzi wake ujao baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Bosnia-Herzegovina ameeleza kuwa wanaelewa umuhimu wa wachezaji wote na lengo ni kufanya maamuzi ya haki na sahihi.

Katika Michuano ya Euro 2024, Uingereza iko Kundi C pamoja na Denmark, Slovenia na Serbia - wapinzani wao wa kwanza huko Gelsenkirchen Jumapili ya 16 Juni mwaka huu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement