Klabu ya Al Hilal kutoka Sudan imewasili nchini Tanzania juzi usiku kwaajili ya maandalizi kuelekea michezo yao Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wanatarajiwa kucheza dhidi ya Petro de Luanda ya Angola ugenini Novemba 25.

Al Hilal walichagua uwanja wa Benjamin Mkapa kuwa uwanja wao wa nyumbani kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutokea kwa machafuko ya kisiasa nchini kwao (Sudan).

Tayari imeanza nmazoezi katika Uwanja wa Uhuru kujiandaa na michezo hiyo na watatumia uwanja wa Mkapa Desemba Mosi kwenye mchezo dhidi ya Espèrance de Sportive de Tunis.

Hilal inakuwa ni timu pekee inayowakilisha Sudan katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya Al Merrikh kutolewa na Yanga katika hatua ya mtoano ya mashindano hayo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement