Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake, JKT Queens, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya wenyeji wa michuano hiyo Athletico FC Abidjan huku Mchezaji wa JKT Quens Donisia Minja akiibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.

Mara baada ya mchezo huo, Afisa Habari wa JKT Queens, Masau Bwire amewashukuru watanzania kwa kuendelea kutoa sapoti kwa timu hiyo ambao wamekuwa moja ya chachu katika kupatikana kwa matokeo hayo.

“Napenda kuwashukuru sana watanzania, mmetuunga mkono, mmetusapoti, mmesababisha matokeo haya chanya kupatikana, mshikamano wetu ulikuwa mkubwa mno, nimeona namna mlivyofuatilia mchezo huu, nimeona namna mlivyokuwa mkishauri japo ushauri wenu haukufika mahala husika, lakini hii yote ni kuonesha kwamba Watanzania tulikuwa pamoja, ” Masau Bwire.

Masau ameeleza kuwa kwa sasa kikosi kinajiandaa na mchezo unaofuata, dhidi ya Sporting Casablanca ambapo ameweka wazi kuwa katika mchezo huo wanahitaji alama zote tatu ili kuweza kukata tiketi ya kufuzu Nusu Fainali ya Michuano hiyo inayoendelea kutimua vumbi nchini Ivory Coast.

Mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya Sporting Club Casablanca itachezwa katika mji wa San Pedro, huku mechi zote za mwisho kundi A zikipangwa kuchezwa wakati mmoja, kuepusha upangaji wa matokeo.

JKT Queens kuanzia alama moja na kuendelea ili kuweza kukata tiketi ya kufuzu Nusu Fainali ya Michuano hiyo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement