HISPANIA YATWAA UBINGWA WA EURO 2024
Timu ya Taifa ya Hispania imeweka rekodi ya kuwa timu iliyotwaa Ubingwa wa Uefa Euro mara nyingi zaidi (mara 4) baada ya kuifunga England magoli 2-1 katika mchezo wa Fainali ya UEFA Euro 2024
Nico Williams alianza kuifungia Uhispania dakika ya 47, Cole Palmer akasawazisha dakika ya 73 kisha Mikel Oyarzabal akafunga goli la ushindi katika dakika ya 86
Matokeo hayo ni mwendelezo wa matokeo mabaya kwa England katika Fainali za michuano hiyo kwa kuwa ilipoteza pia Fainali zilizopita za Mwaka 2020 kwa kufungwa na Italia kwa penati



