Hermoso akanusha kutoa ridhaa ya kupigwa busu na Rubiales
Kikosi cha mabingwa wa dunia cha wanawake cha Uhispania kimetishia kutocheza tena endapo mkuu wa shirikisho la soka la nchi hiyo RFEF Luis Rubiales hatojiuzulu.
Rubiales amekataa kujiuzulu baada ya kutuhumiwa kwa wiki nzima kufuatia hatua yake ya kumbusu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake Jenni Hermoso baada ya ushindi wao wa Kombe la Dunia.
Baadaye mchezaji huyo alikanusha kwa hasira madai ya Rubiales kwamba alitoa ridhaa ya kupigwa busu. Baraza la juu la michezo la Uhispania CSD limetangaza kwamba linalenga kumsimamisha kazi.
Shirikisho la soka duniani FIFA lilianzisha uchunguzi wa kimaadili kuhusu tukuio hilo huku chama cha wachezaji FIFPRO kikishinikiza shirikisho la soka Ulaya UEFA, nalo kuchukua hatua kama hiyo. Rubiales ni miongoni mwa makamu wa rais wa UEFA