Henderson aliweza kuibuka kibabe katika changamoto ya mikwaju ya penati ambazo zilipigwa kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.


Kipa huyo aliokoa penati mbili za wachezaji wa Liverpool zilizopigwa na Alexis MacAllister na Harvey Elliott huku Mohamed Salah yeye akipaisha penati yake juu ya lango na hatimaye Crystal Palace kuandikisha ushindi wa penati 3-2.



Lakini, wakati penati zinapigwa, kamera za uwanjani zilimuonesha Henderson akichungulia chupa yake ya maji iliyobandikwa karatasi yenye maelezo na kuifunika kwa kitaulo chake.


Karatasi hiyo ilikuwa na majina ya wapiga penati wote wa Liverpool na wapi wanapopenda kuzielekeza penati zao.


Kwa mujibu wa picha ya karatasi hiyo inavyoonekana, orodha hiyo ilikuwa na majina ya wapiga penati tisa (9) wa Liverpool ambao ni Ibrahima Konate, Andy Robetson, Cody Gakpo, Dominik Szoboszlai, Alexis MacAllister, Curtis Jones, Virgil van Dijk, Salah na Elliott.


Na katika wapigaji watano wa Liverpool, Henderson aliokoa za Salah na Elliott huku Szoboszlai na Gakpo wakifanikiwa kuepuka kizingiti hicho, ingawa jitihada zao hazikuisaidia timu yao kuibuka na ushindi.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement