HALI ILIVYO NJE YA UWANJA WA ANFIELD BAADA YA KIFO CHA DIOGO JOTA
Mashabiki wa soka wakiwemo wa Liverpool na klabu mbalimbali wamejitokeza nje ya uwanja wa Anfield unaomilikiwa na Klabu hiyo wakiwa na maua wakiombeleza kifo cha mchezaji wa klabu hiyo kilichotokea alfajiri ya leo Diogo Jota.
Klabu ya Liverpool imeshusha bendera yao Nusu Mlingoti kwa heshima ya mshambuliaji huyo aliyekuwa anavaa jezi namba 20.Jota ambaye amefariki kwa ajali ya gari Nchini Hispania akiwa na mdogo wake Andre Silva Jota alijiunga na Majogoo wa Jiji la London mwaka 2020 na kuisaidia klabu yake kushinda ubingwa wa 20.



