Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) huenda likalazimika kuilipa klabu ya Al-Hilal kitita cha pauni milioni 6.5 (≈ Tsh bilioni 20) baada ya mshambuliaji wa Brazil, Neymar Jr kupata jeraha akiwa kwenye majukumu ya kimataifa na Brazil ambalo litamuweka nje ya uwanja kwa msimu mzima.

Neymar anayekipiga Al Hilal ya Saudi Arabia alilazimika kutolewa nje kwa machela katika kipindi cha kwanza cha kipigo cha Brazil cha 2-0 dhidi ya Uruguay huku klabu hiyo ikithibitisha kwamba nyota huyo amepata jeraha la anterior cruciate ligament (ACL) na atalazimika kufanyiwa upasuaji.

Shirikisho la soka duniani lina sera ya bima, FIFA Club Protection Program (CPP), ambayo italipa mshahara wa mchezaji kutoka siku 28 hadi mwaka na kiwango cha juu cha £6.5m iwapo atajeruhiwa akiwa kwenye majukumu ya kimataifa.

Hata hivyo Neymar aliyejeruhiwa ataigharimu Al-Hilal zaidi ya pauni milioni 6.5 kwal kuwa Mbrazil huyo yuko kwenye mkataba ambao utagharimu pauni milioni 276 kwa kipindi cha miaka miwili

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement