Felix Sunzu Amesema, katika eneo la ushambuliaji kwa kumuanzisha Jean Baleke na kumtosa John Bocco ambaye amekuwa akiaminiwa siku za hivi karibuni.

Simba itakuwa mwenyeji wa Al Ahly katika mchezo wa African Football League utakaopigwa jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kisha kurudiana Oktoba 24, Cairo, Misri.

Sunzu, raia wa Zambia alisema hana wasiwasi na Simba kushinda mbele ya Waarabu hao katika uwanja wa nyumbani ambapo wamekuwa na faida mara nyingi, lakini hofu yake ni mchezo wa marudiano ugenini, hivyo benchi la ufundi linapaswa kumaliza kazi nyumbani kwa kufanya uamuzi sahihi.

Alisema Baleke ana uwezo mkubwa wa kufunga, kutuliza mali na ana bahati kwenye michuano mikubwa ya Afrika kuliko Bocco, huku akishauri kama asipofanya yanayotarajiwa basi yafanyike mabadiliko chapu aingie Moses Phiri. “Pale eneo la mbele hakuna mtu wa kutunza mpira muda mrefu wakipata mtu kama huyo hata ligi wanachukua mapema.

Bocco amekuwa akipata nafasi kubwa ya kucheza lakini kiukweli siyo mtu wa kumuanzisha katika mechi hii labda wamuangalie Baleke asipofunga aingie Phiri, alisema Sunzu. "Baleke aanze kwa sababu amekuwa na nafasi kubwa ya kufunga kwenye Ligi ya Mabingwa

msimu uliopita katika mechi muhimu. Mchezaji wa hivyo siyo wa kumuweka benchi naamini akiaminiwa kwenye mchezo huu atafunga." Alishauri mabeki wa pembeni kutofanya makosa yaliyoonekana kwenye Ligi Kuu na kuwataka waongeze umakini sambamba na

kutofanya kosa eneo la ulinzi na kipa, kutowapa nafasi (kutia presha) na kuhakikisha wanawachosha wapinzani wao. Nina wasiwasi na kuanzishwa Aishi Manula kwenye mchezo huu kwa sababu ametoka kwenye majeraha lakini ni kipa mzuri anayeweza kuisaidia timu, lakini kipa atakayepangwa atulize mabeki, aongee awe mzuri kwenye kuanzisha mipira, kwa hiyo hata huyo Salim (Aly) ni kipa mzuri anaweza tu kucheza" alisema Sunzu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement