Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco imevuliwa ubingwa wa ligi Kuu Morocco na FAR Rabat ambao ndio Mabingwa wapya wa Ligi hiyo kufuatia ushindi wa wa 3-2 dhidi ya IR Tanger.

Wydad AC wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Maghreb Fez FC lakini wameukosa ubingwa kwa tofauti ya alama moja.

FAR Rabat walihitaji penalti ya dakika za lala salama kupata alama tatu zilizowapatia ushindi na ubingwa huo.

FAR Rabat imetwaa ubingwa wake wa 13 Kihistoria kwenye Ligi kuu Nchini humo ikiwa ni ubingwa wa kwanza tangu 2008.

MSIMAMO πŸ” TWO

πŸ₯‡FAR Rabat mechi 30 - alama 67

πŸ₯ˆ Wydad AC mechi 30 - alama 66

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement