Baada ya kutumika kwa dakika 630 na kuisaidia timu yake kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara, kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra amekiri ligi ni ngumu huku akifunguka CAF imempa ubora.

"Msimu huu ni mgumu sana. Sina mwanzo mzuri kama msimu uliopita. Hadi sasa kwenye mechi saba nilizokaa langoni nimeruhusu nyavu zangu kutikiswa mara tatu, lakini hilo halinivunji moyo kwani nina imani kubwa na ukuta unaonilinda" alisema

Diarra ambaye ana 'clean sheet' nne hadi sasa. "Na nimerudi na nguvu mpya kwa kuamini kuwa kupoteza 'clean sheet' ni sehemu ya mchezo. Nitaendelea kujifua na kupunguza makosa kwenye mechi zilizo mbele nia ni kuisaidia safu yangu ya ulinzi kulinda ushindi tunaoupata."

Akizungumzia kutajwa kwenye tuzo za CAF, Diarra alisema sio jambo dogo kwake linamuongezea nguvu za kujiamini na kufanya mambo makubwa zaidi ili kuendelea kujiweka kwenye ushindani na makipa wakubwa. "Ubora wangu umeonekana uwanjani kutajwa sambamba na makipa wa timu kubwa. Kwangu ni ushindi ligi ina timu 16 mimi peke yangu kwa Tanzania ndiye nimeonekana. Huu ni ushindi mkubwa kwangu," alisema.

"Tayari najiona mshindi, makipa kumi barani Afrika jina langu lipo sio kitu kidogo. Nimepata nguvu na kupata imani kuwa kila kitu kinawezekana na nitaendelea kuwa bora zaidi ya hapa nilipo sasa kutokana na kuamini kuwa natazamwa na wengi na ubora wangu umekuwa Darasa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement