CRISTIANO RONALDO HAAMINI KILICHOTOKEA KUHUSU KIFO CHA NYOTA JOTA
Kifo ni fumbo gumu mno. Sio rahisi kupata jibu lake na ndio maana tunashauriwa kushukuru hata pale tunapompoteza yule tuliyempenda na kumfurahia kila tulipomuona, kwa maana kilio pekee hakitasaidia arudi.
Lakini katika mazingira ya kawaida na kiubinadanu, mshituko ni lazima utokee kwa mtu yeyote, ndio hiki kinachotokea sasa kwa nyota wa Al Nassr na nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo kuonesha wazi namna alivyoshitushwa na msiba wa mchezaji mwenzake timu ya taifa;
"Haiingii akilini. Tulikuwa wote timu ya taifa (hivi karibuni) na ulitoka kufunga ndoa na mke wako...".
“Nitoe salamu za rambirambi kwa familia yako, mke wako na watoto wako...najua utakuwa pamoja nao wakati wote (kiroho)."
“Pumzika kwa amani, Diogo pamoja na Andre (mdogo wa Diogo). Tutawakumbuka milele," ameandika Ronaldo kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram.



