Nyota wa kimataifa wa soka la wanawake, Clara Luvanga anayekipiga Al Nassr ya Saudia Arabia amechaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, huku akitaja ushindani wa tuzo hiyo.

Ni siku 26 sasa zimepita tangu Clara ajiunge na kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu nchini humo Oktoba 19 mwaka huu na amekuwa na mchango mkubwa sana.

Clara anayewania tuzo hiyo na nyota mwezake Lina Busaha na Ashleigh Plumptre wa Al Ittihad kila mmoja akiwa amecheza mechi nne, huku Clara akiwa amecheza dakika 282 na kufunga mabao manne, Lina akicheza dakika 315 akifunga pia manne na Ashleigh amecheza dakika 341 na kufunga mabao matatu.

Clara alisema amefurahi kuchaguliwa kuwania tuzo hiyo lakini anawaomba Watanzania wamsapoti kwa kumuombea afike mbali kwani ushindani ni mkubwa. "Ukiangalia wote tuliochaguliwa hapo ni wazuri, kikubwa sapoti ya Watanzania kunipigia kura ili nishinde naamini nitafanya makubwa," alisema Clara.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement