Cavani, Suarez Waondoshwa Kikosini Uruguay
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Uruguay Marcelo Bielsa amefanya chaguzi ya wachezaji wenye umri mdogo kuitumikia timu ya Taifa katika mechi za kuwania kufuzu kushiriki kombe la Dunia la mwaka 2026.
Wakongwe Luis Suarez pamoja na Edison Cavani wote wakiwa na umri wa miaka 36 hawajajumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Uruguay.
Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 2007 Edison Cavani pamoja na Luis Suarez kutojumuishwa kwenye kikosi cha timu yao ya Taifa Lao.
Uruguay siku ya Jana wamecheza na Chile na wamefunga magoli 3-1.
Magoli yao yamefungwa na mchezaji Nicolaus De La Cruz aliyefunga magoli 2 pamoja ja Federico Valverde na goli la Chile likifungwa na Artulo Vidal