BRAZIL KUWA MWENYEJI WA KOMBE LA DUNIA LA WANAWAKE 2027
Katika Kongamano la 74 la Shirikisho la Soka Ulimwenguni “FIFA” huko Bangkok, Thailand, Brazili imetangazwa kuwa nchi mwenyeji wa Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake la kumi litakalofanyika mwaka wa 2027, na kuwa taifa la kwanza la Amerika Kusini kuandaa mashindano hayo.
Tangazo hili linakuja baada ya mchakato mpana zaidi wa zabuni ya Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake kuwahi kutokea, na kwa mara ya kwanza kabisa kuamuliwa kupitia kura ya wazi katika Kongamano la FIFA ambapo Brazil ilipata kura 119 huku zabuni ya pamoja ya Ubelgiji, Uholanzi na Ujerumani ikipata kura 78.
Mashindano hayo yatatoa fursa muhimu kwa FIFA kuendelea kuendeleza kasi iliyotokana na matoleo yaliyopita, ikiwa ni pamoja na Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake la 2023 lililofanyika nchini Australia na Aotearoa New Zealand na kupongwezwa kwa kuvunja rekodi.