baada ya mchezaji huyo wa klabu ya Al-tihad ya Uarabuni, kuonyesha kuunga mkono Taifa la Palestina katika mzozo wao na Israel, siku za hivi karibuni.

Benzema alitumia ukurasa wake wa Twitter kuandika ujumbe uliosomeka;

"Maombi yetu yawafikie wakazi wa Gaza ambao kwa mara nyingine ni waathirika

wa milipuko hii yenye kukiuka ubinaadam, ikiwaathiri wanawake na watoto."

Baada ya Ujumbe huo, mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid, alipokea

ukosoaji mkubwa kutoka kwa watu mbalimbali.

GĂ©rald Darmanin, alidai katika mahojiano ya televisheni kwamba,

"Kama sote tujuavyo, bwana Karim Benzema ana uhusiano hatari na kundi la

Muslim Brotherhood."

Vilevile, Kipa wa zamani wa Jsrael, na klabu ya Mallorca, Dudu Aouate pia

alitumia ukurasa wa Twitter kumtusi Benzema katika lugha tano tofauti, na

kupelekea chapisho hilo kuzuiliwa na Twitter, kufuatia matumizi ya lugha chafu.

Tofauti na majanga mengi ya awali limwenguni, suala hili kati Israeli na

Palestina limeugawa ulimwengu wa soka, hatua inayozua hali ya utata pindi

wachezaji wanapojaribu kuonyesha kuunga mkono upande fulani na kusababisha

baadhi ya wachezaji, kama vile Benzema, kukosolewa kwa lugha kali.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement