Taifa la Argentina leo limeweka rekodi mpya baada ya kushinda fainali ya Copa America, kuifunga timu ya taifa ya Colombia bao 1 kwa sifuri kwenye dakika 30 za nyongeza na Argentina kubeba kombe hilo

Bao hilo lilifungwa na mchezaji wa inter Milan Lautaro Martinez dakika ya 112 akipokea pasi nzuri kutoka kwa Le celso na KUFUNGA bao lake la 5 la mashindano nakua mfungaji Bora 

Rekodi mpya iliyowekwa ya kwanza ni kua taifa lililo fanikiwa Zaidi kuchukua kombe hili mara nyingi Zaidi kuliko timu yoyote ile na sasa wabeba mara 16 mbele Zaidi ya Uruguay ambao wao mara 15 tu

Lakini rekodi nyingne imekua taifa la kwanza kutokea Amerika ya kusini kubebe makombe matatu makubwa mfululizo yaani Copa America 2 na kombe la dunia 1 ndani ya fainali 3 mfululizo lakini pia wamevunja unbeaten ya Colombia baada ya Kucheza MICHEZO 28 bila kupoteza Sasa Argentina imeivunja kwenye Mchezo wa 29

Leo Messi amechukua taji la 2 la Copa America katika FAINALI 4 zilizo pita kitu ambacho kimempa heshima nyingne katika maisha yake ya soka 

Lakini Angel Di maria umekua ndo mchezo wake wa mwisho na jezi ya Argentina akiwa ameifungia taifa hilo mabao 31 na rasmi amestaafu timu ya TAIFA 

Baada ya Argentina kuchukua fainali hii ni rasmi ataenda kukutana na taifa la Spain katika FAINALI ya Finalisma ambapo watakutana mwakani

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement