Rebbach ana ndoto za kuchezea timu ya taifa. Winga wa klabu ya Deportivo Alaves, Abde Rebbach amesema anatamani kujiunga na timu ya taifa ya Algeria.

''Unapocheza katika ligi ya kiwango cha juu, ungependa kila mara kujiunga na timu ya taifa. Na ninatumai nitapokea wito wa kujiunga na timu ya taifa ya (Algeria)'' alisema Abde Rebbach, winga wa Deportivo Alaves.

''Timu (Deportivo Alaves) inacheza vizuri. Niko tayari kuwasaidia katika kipindi cha mwisho cha msimu, na kufanya kile kinachohitajika ili timu iendelee kufanya vyema,” Rebbach aliongeza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amefunga mabao 4 katika mechi 29 za La Liga.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement