Yanga Yamaliza Mechi Ugenini,Yahinda 2 Dhidi Ya Al Merrekh
Safari ya klabu ya Yanga SC kuelekea hatua ya makundi kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika wameanza vyema wakiwa ugenini kwa kuifunga klabu ya Al Merrekh ya Sudan magoli mawili
Kennedy Musonda ndio alifungua kitabu cha magoli kwa Yanga katika dakika ya 63 kabla ya Clement Mzize kufunga kitabu dakika ya 80 kwa kuweka goli la pili. Kwa matokeo hayo sasa Yanga wanahitaji sare ya aina yoyote katika mchezo wao wa marudiano ili kuweza kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika msimu wa 2023-2024.