Mechi za ligi daraja la kwanza zimeendelea leo hii kwa Polisi Tanzania kucheza na Ruvu Shooting katika uwanja wa Ushirika uliopo mkoani Kilimanjaro,katika mchezo huo Polisi Tanzania wamefanikiwa kuondoka na alama zote tatu kwa goli pekee lililofungwa na Denis Mushi dakika ya 15.

Kwa matokeo hayo Polisi Tanzania wanakuwa wamejikusanyia alama nne katika michezo miwili baada ya mchezo wa kwanza kutoa sare dhidi ya Mbeya Kwanza,wakati huo huo Ruvu Shooting wanaendelea kupoteza mechi zao baada ya mchezo wa kwanza ambao walipoteza FGA TALENTS.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement