RATIBA MECHI YA MCHUJO WA KUSHUKA/KUPANDA DARAJA

MBEYA CITY vs MASHUJAA FC (Agg. 1-3)

🏟️ Sokoine, Mbeya

⌚ saa 10:00 jioni


Pazia la michuano ya mchujo (playoff) ya kushuka/kupanda daraja linafungwa leo kwa mchezo mmoja wa kuamua timu itakayoshiriki Ligi Kuu ya soka Tanzania bara msimu ujao.


Mbeya City iliyokubali kipigo cha 3-1 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Lake Tanganyika inahitaji ushindi mkubwa leo katika dimba la Sokoine ili kupindua meza na kusalia Ligi kuu huku Mashujaa wakihitaji walau sare au kipigo cha bao 1-0 kukata tiketi.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera alitangaza kiingilio kwenye mechi hiyo kuwa ni bure huku Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye akijibu mapigo kwa kutangaza kununua kwa Tsh laki 6 kila bao litakalofungwa na Mashujaa.


✍️ Ni mpambano mkali kati ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya dhidi ya mkuu wa Mkoa wa Kigoma.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement