Klabu ya Arsenal imeanza rasmi kampeni yake ya kusaka ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza leo hii kwa kuichapa Nottigham Forest 2-1. Mchezo uliochezwa jijini London katika uwanja wa Emirate, Arsenal ndo walikuwa wakwanza kupata mabao mawili kupitia washambuliaji wao Saka na Nketiah dakika ya 26 na 32 kabla ya Nottingham kupata bao lao dakika ya 82

Kwa matokeo haya yanawafanya Arsenal kuanza vizuri safari yao katika kusaka ubingwa ambao walikaribia kuupata msimu uliopita baada ya kufanya vyema lakini Manchester City waliweza kubeba taji hilo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement