The Open Championship 2025 inaanza Royal Portrush
Uwanja wa Dunluce Links, ndio uwanja utakao tumika kwenye ufunguzi huu ,uwanja huu unasifa mbali mbali zikiwemo umbali wa futi 7,381 (par 71), umeboreshwa tangu 2019, ikiwemo kuimarishwa kwa bunkers na kuongeza changamoto mpya kama “Calamity Corner” kwenye hole ya 16.Ni uwanja mgumu, wenye upepo mwingi, mwinuko na kutofautiana kwa juu na chini, ukiwa ukilazimisha mbinu thabiti ya wachezaji .
Hakika haya mashindano ya kihistoria ya golf ya The Open 2025 yanaanza leo huko Royal Portrush, Ireland Kaskazini (Julai 17–20). Mchezaji mwenyeji Rory McIlroy, aliyejishindia Career Grand Slam kwa kushinda Masters hivi karibuni, anatazamiwa kudhibiti eneo lake la nyumbani na kupigania Claret Jug tena. Mshindi wa mwaka uliopita, Xander Schauffele, pamoja na wachezaji wengine maarufu kama Scottie Scheffler, Shane Lowry, Jon Rahm, na Brooks Koepka, wanaingia dimbani kwa matarajio makubwa. Leo utashuhudia wave ya mchezo wa awali (Round 1) kuanzia alfajiri, huku mashabiki 278,000 wakitarajiwa kushuhudia tukio hilo futari. Utangazaji unafanyika kupitia talkSPORT 2 na Sky Sports Golf