Timu ya Taifa ya Ivory Coast ambao ni wenyeji wa AFCON 2023 imefanikiwa kwenda hatua ya robo fainali kwa kuwatoa Mabingwa watetezi Senegal kwa mikwaju ya penati 5-4 na sasa Ivory Coast sasa itacheza robo fainali na Mshindi wa mechi ya Mali na Burkinafaso ambayo itachezwa kesho.

Wengi hawakutarajia kama Ivory Coast anaweza kuiondoa Senegal katika mashindano haya kutokana na Ivory Coast kusuasua na hata kuingia hatua ya 16 bora kama best loser baada ya kushinda mechi moja tu ya makundi na kupoteza mechi mbili.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement