Kiptum ambaye anashikilia rekodi ya kihistoria ya mwanariadha mwenye kasi zaidi katika historia ya mbio za masafa marefu amefariki pamoja n kocha wake, Gervais Hakizimana, katika ajali ya gari siku ya Jumapili usiku (11 Februari) kwenye barabara ya Eldoret-Kaptagat.

Iliyoidhinishwa na Shirikisho la riadha duniani (IAAF) limeidhinisha rekodi ya kihistoria ya dunia iliyowekwa na mwanariadha wa mbio za masafa marefu raia wa Kenya Kelvin Kiptum.

Mkenya huyo alivunja rekodi ya mbio za marathon za wanaume mjini Chicago tarehe 8 Oktoba 2023, kwa muda wa saa mbili na sekunde 35 ambapo alipunguza sekunde 34 kutoka kwa rekodi ya awali ya bingwa wa Olimpiki mara mbili Eliud Kipchoge kutoka Berlin mwaka jana na kuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia marathon chini ya saa mbili na dakika moja ambapo IAAF iliidhinisha rekodi yake ya dunia wiki iliyopita tu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement