Timu ya Taifa ya Kenya imeanza vizuri kampeni yake ya kuwania Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) kwa wachezaji wa ndani kwa kuwalaza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR CONGO) 1-0 katika mechi ya ufunguzi ya Kundi A ulifanyika katika Uwanja wa Kasarani jijini Nairobi.

Mpambano huo ameuhudhuriwa na Rais wa Kenya William Ruto, na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe na kiongozi wa ODM Raila Odinga ambapo bao la pekee la mechi hiyo lilitoka kwa kiungo Austin Odhiambo, ambaye alifunga bao zuri la mguu wa kushoto katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza (47’), na kupata alama tatu muhimu kwa Harambee Stars.


You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement